UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ?
MAKALA
hii nimeiandika maalumu kwa watanzania na
wadau wangu wote , wanafunzi wa SHULE ZA MSINGI ,
SEKONDARI, na VYUO wanaopenda kujifunza
LUGHA YA KIINGEREZA AU KISWAHILI na lugha
nyingne ngeni lengo ni kuweza
KUANDIKA na KUONGEA kwa UFASAHA na UMAHIRI.
Limekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania wengi na
wanafunzi wetu kuanzia ELIMU AWALI, MSINGI,SEKONDARI , VYUO
kutoweza kuongea KIINGEREZA kwa
ufasaha na umahiri.Hata Lugha ya
KISWAHILI ingawa ni lugha yetu
ya taifa bado ni tatizo kwa
watanzania wengi na wanafunzi kuongea
kwa ufasaha na umahiri ! TATIZO NI NINI ?
UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ? Kujifunza
LUGHA yoyote ni suala ENDELEVU {long
and permanent term } na siyo suala la
KUJIFUNZA LUGHA KWA WIKI TATU TU,
AU MIEZI MITATU TU ,AU MIEZI
SITA TU ! KAMA MATANGAZO YA BIASHARA
YANAVYOJITANGAZA . “ JIFUNZE LUGHA YA
KIINGEREZA KWA WIKI TATU “ hii
si kweli ndugu yangu.
LUGHA ni mtaji , inaweza kukufanikisha
mambo yako katika maisha ! Ndugu
yangu MTANZANIA kama wewe ni
mbumbumbu wa Lugha ya KISWAHILI
au KIINGEREZA utachina au
utakwama katika masuala
yako yanayohitaji UMAHIRI katika
lugha hizo mbili . Kuna umuhimu
sana kwa ndugu yangu MTANZANIA
kuwa MAHIRI katika kutumia KISWAHILI
au KIINGEREZA kwa ufasaha na umahiri .
SIRI
ZA KUIKUZA LUGHA YA
KIINGEREZA
---Huwezi kuimiliki lugha yoyote
kama huitumii.Mtu anaweza kujidai kuwa
kwa vile ni mswahili na
amezaliwa katika lugha hii basi
anaijua lugha. Hii si kweli kabisa
ndugu yangu .Kama ingekuwa hivyo basi
wote tungeweza kutumia na kuielewa
MISAMIATI na MISEMO yote ambayo
iko katika lugha yako.Kwanini basi
wengine wakiitumia MISEMO na
MISAMIATI hito wewe unatoka kappa ,
ni kwa sababu huitumii.Kwa hiyo jambo
la msingi ni kuhakikisha kuwa
unaitumia lugha.
----Kwa wale wanaojifunza
lugha ya kigeni , jambo la msingi ni
kuhakikisha kuwa unaitumia ili uweze
kupata uzoefu na hatimaye kuitumia
kadri unavyotaka.
-----KUITUMIA
LUGHA MAANA YAKE NINI ? Izungumze au itumie
katika MAANDISHI ; kama ni lugha
ngeni kwako.Kadri unavyoendelea kuitumia
katika mazungumzo au katika kuiandika
basi unakuwa na uwezo wa
kuielewa na utahitajika kupata
misamiati mipya.
----Hudhuria katika mikutano na
uhakikishe unatafuta nafasi ya
kuzungumza. Unapozungumza katika matukio
kama hayo maana yake utapaswa
kuchagua MANENO/ MISAMIATI na kuyapanga
ili uonekane unajieleza kwa ufasaha
na kile kinachokusudiwa. UWEZO WA
LUGHA UTAHITAJIKA.
-----Makongamano , au hata ubishi
wa kawaida mitaani ni nafasi
nzuri kwako wewe kuitumia ili
uweze kukuza uwezo wako wa lugha. Na
wewe uingie katika ubishi
halafu uangalie , fanya tathmini , baadaye , kwa
nini ulishindwa au kushinda, kwa
nguvu ya hoja au kwa hoja
ya nguvu.Kama unamiliki lugha
unaweza KUSHINDA kila KONGAMANO.
-----Jifunze kutunga HADITHI
au kuzisoma , KUTUNGA MASHAIRI.Haya ni
mambo pekee yanayoweza kukufanya
uhitaji uwezo mkubwa wa lugha
na hazina kubwa ya MISAMIATI.
UTATUNGAJE
MASHAIRI KAMA MISAMIATI
YAKO NI MICHACHE ?
Aidha
ukitunga MASHAIRI au HADITHI
utajikuta nyakati zote unatafuta
KAMUSI au VITABU vya
MISEMO na lugha ili uweze
kupata MANENO yanayofaa katika utunzi
wako kwa ajili hii LUGHA yako
inakua kwa haraka sana.
Lakini zuri sana hapa ni
kuwa kadri unavyoendelea kujihusisha
na utunzi wa MASHAIRI au HADITHI
UNATUMIA MUDA MWINGI KUFIKIRI ,
na jinsi unavyoendelea kushughulika
na mambo hayo, uwezo wako wa KUFIKIRI
NA KUTAFAKARI nao huongezeka. Ongezeko la
uwezo wako wa KUFIKIRI ni
matokeo ya kuwa na UWEZO
MKUBWA WA LUGHA.
----SIKILIZA , Wengine hudhani
KUSIKILIZA sio sehemu ya kutumia /
kujifunza LUGHA.
-----FUNGULIA REDIO, utasikiliza
MISEMO na MISAMIATI mbalimbali
ambayo utahitajika kuielewa ili
uweze kufuatilia kinachoelezwa .Kwa
hiyo basi kadri
unvyoendelea kuisikiliza ndivyo
unavyoweza kuielewa vizuri zaidi.
Kwanza unapoisikiliza lugha
ikizungumza na wenyewe ,
kwa mfano , unajifunza MATAMSHI SAHIHI ,
unajifunza MISEMO ambayo huwezi
kuipata katika matukio mengine.
Unatakiwa kuwa mwangalifu katika
kuchagua vipindi , kama unachagua redio
au televisheni ; kuna TAARIFA YA
HABARI ambayo , hutumia LUGHA RASMI ili uweze
KUJIFUNZA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA
REJISTA MBALIMBALI ZA LUGHA.
Lakini chagua vipindi vya DRAMA
, yaani MICHEZO YA KUIGIZA. Utajifunza
LUGHA ikizungumzwa katika
mazingira yake halisi--- NATURAL SETTING. Matamshi ,
mwitiko na uteuzi wa lugha
unaondana na mazingira.SIKILIZA
VIPINDI VYA DINI , SHULE , SAYANSI , UCHAMBUZI
na kadhalika ili uweze kupata
MISAMIATI MBALIMBALI KWA AJILI
YA KUKUSAIDIA.
HITIMISHO
----Kama unajifunza LUGHA YA
KIGENI , fanya marudio , mazoezi mengi na soma
vitabu vingi vya hadithi vya lugha
hiyo.
-----Soma ukiwa na KAMUSI
na tafuta maana ya neno usilolijua.
----Jizoeze KUSIKILIZA na KUONGEA
ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
-----Sikiliza MIHADHARA na
REDIO ili ujifunze kwa
wengine wanavyotamka maneno.
-------Jikumbushe MANENO
magumu kila siku.
------Kila nafasi
unayoipata itumie kwa kusoma.
------Pambana na SARUFI za
LUGHA YA KIGENI kikamilifu.
------Jifunze lugha ya kigeni
kwa kuongea mara kwa mara.
Asante
sana wadau wangu hasa WANAFUNZI
wangu kwa kusoma makala
hii nzuri sana kama utaweza
mwonyeshe mwenzako naye asome apate
kuelewa jinsi ya kukuza lugha
ya kiingereza na lugha nyingine.